Bawasiri ni kuvimba kwa mishipa ya damu iliyopo ndani ya au katika eneo linalozunguka njia ya haja kubwa. Ni hali ambayo inaweza kusababisha nyama kujitokeza nje. Hivyo bawasiri inaweza kuwa bawasiri ya ndani au bawasiri ya nje. Ugonjwa huu unaweza kusababisha mwasho, maumivu na damu au kamasi kutoka wakati wa kujisaidia haja kubwa ingawa wakati mwingine hauna dalili. Madhara ya bawasiri ya ndani ni pamoja na damu kutoka wakati wa kujisaidia, damu kuganda ndani ya mishipa ya damu na maumivu.
Kutokea kwa bawasiri kunaweza kuhusishwa na hali kama uzee, ujauzito, kuharisha au choo kufunga (constipation), saratani kwenye nyonga au kukaa kwa muda mrefu. Tiba ya bawasiri inategemea aina ya bawasiri na ukubwa wa tatizo. Matibabu ya bawasiri yanaweza kuhusisha matumizi ya dawa au upasuaji mdo