Kisukari ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu inapokuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda murefu.
Ugonjwa wa kisukari husababishwa na kongosho kutoweza kutoa kiwango cha insulini mwilini kinachofaa. Pia yaweza kuwa mwili haufanyi kama unavyotarajiwa kufanya insulini ikifika sehemu ile ya mwili.
Kuna aina tatu za Kisukari:
1-Moja ni wakati kongosho imeshindwa kutengeneza insulini kiwango kizuri cha kudhibiti sukari mwilini
2-Aina ya pili ni wakati mwili unakataa kudhibiti sukari hata insulini ikitengenezwa na kongosho
3-Aina ya tatu ni bolisukari ambayo huathiri wanawake wajawazito ambao hupata kwamba kiwango cha sukari miilini mwao kimekwenda juu hata kama hawana historia ya aina hii.
Dalili za kisukari ni
kukojoa kupita kiasi cha kawaida
kiu kubwa
kuona vibaya na matatizo ya macho hadi kuwa kipofu
kuchoka haraka
vidonda vinavyopoa polepole mno, hasa kwenye miguu, hadi kupotewa na viungo